KUNA mastaa ambao walijikuta wakiwaacha wengi midomo wazi kutokana na kuwa na miili iliyoshiba lakini ghafla wakaonekana katika muonekano tofauti wakiwa ‘wamepukutika’ na kuzua viulizo, huku wengi wao wakitoa visingizio mbalimbali.

GIGY MONEY
Mwanadada huyu anayejulikana kwa jina halisi la Gift Stanford alitikisa mno kwa muonekano wake, jinsi alivyokuwa amenona na kujazia kwenye msambwanda, lakini kitu kilichowaacha wengi hoi ni baada ya kupukutika ghafla, huku sababu mbalimbali zikitajwa,
ikiwemo kuharibika kwa mimba kadhaa na `stress’ za mapenzi na hadi sasa mwili wake haujarudi.


AUNTY LULU
Ni moja ya wadada ambao walikuwa gumzo kila kona, huku mara kadhaa akijitapa kuwa wowowo lake ndo kila kitu maishani mwake, lakini siku chache zilizopita mwanadada huyo aliibua
taharuki baada ya kuonekana akiwa modo na kalio limeiisha, huku akidai ni kutokana na kufanya mazoezi, hivyo mpaka sasa hajarudi kwenye ubora wake.

AMANDA
Msanii huyo alikuwa balaa kwenye suala zima la mvuto, mwili na shepu yake alikuwa amefungasha vilivyo, lakini jambo lililoibua taharuki ni baada ya kupungua huku watu wakimzushia mambo mbalimbali ikiwemo maradhi ya kisasa, jambo alilolipinga
vikali, ila hadi wakati huu ameshindwa kurejea kama zamani.

BABY MADAHA
Bishosti huyu ambaye naye alikuwa kibonge mwepesi lakini ghafla akapukutika, huku mwenyewe akidai ameamua kuwa modo sababu anaupenda mwili huo kuliko akiwa bonge na hadi sasa amebaki katika hali hiyo ya umodo. RAY C Anaitwa Rehema Chalamila ni moja ya wasanii wenye sauti mwanana ya kumtoa nyoka pangoni, bibie huyo kipindi kifupi cha nyuma alikuwa kibonge na kuonyesha kutopendezwa na muonekano huo akawa anajitahidi kufanya mazoezi mara kwa mara ili apungue na akafanikiwa, hadi sasa amebaki kwenye hali hiyo ya wembamba.

AMBER LULU
Jina lake halisi ni Lulu Euggen `Amber Lulu’ kwa wanaomfahamu vyema mwanadada huyu machachari, watakubaliana na mimi kwamba siyo Amber yule, alikuwa ana mwili
wa haja na kajazia kinoma kwenye msambwanda, saizi imebaki stori tu.
Na MAYASA MARIWATA 

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com