WANASEMA WBC ndio sehemu ambayo burudani nzuri huwa inatoka kwa sana, lakini pia ndio sehemu ambayo inaongoza kwa drama nyingi sana kuanzia skendo za hapa na pale na mambo mengine mengi.

Ni Wcb, ambapo wakati ishu ya Harmonize na Wolper ikiwa bado haijapoa huku nako Rais wao Diamond Platnumz ishu bado inazidi kuwa tat asana.

Hakuna asiejua suala la uwepo wa tetesi juu ya mgogoro kati ya Diamond na mwenza wake Zari ambapo jana katika picha aliyoweka Instagaram Diamond, mwenza wake huyo Zari aliweka maoni yake kwa kuweka emoji ya kuonesha kidole cha kati.

Pengine unaweza hisi labda alikosea lakini alifanya hivyo mara mbili hiyo kuonesha msisitizo zaidi kwa kitu alicho komenti.

Uwepo wa mgogoro baina yao ulianza kipindi ambacho inasemekana Diamond alitembea na mwanadada Hamisa Mobetto ambaye alipata ujauzito unaodaiwa kuwa ni wa Diamond.

Ishu ikazidi kuwa tamu zaidi baada ya Mobetto kujifungua na kuamua kumpa mtoto jina lake Nassib ambalo ndio jina halisi la Diamond.

Pia mwanzoni ilibainika kuwa mahusiano ya Mama Diamond na Zari si mazuri na hivyo kuzidi kuhatarisha zaidi penzi la hao watu wawili ambalo limeweza kudumu kwa kipindi kirefu zaidi.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com