Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amemtembelea Hospitali alikolazwa Mbunge na Mwanasheria wa CHADEMA Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi Dodoma ambapo baada ya kufika, ametueleza hali ya Tundu Lissu pamoja na anachohitaji Watanzania wafanye.

Japo hakuwa na uhakika kama Madaktari wangeruhusu kwenda kumsalimu Tundu Lissu, ruhusa ilitoka baadae ambapo baada ya kumuona na kuagana nae, Nyalandu amesema yafuatayo

MUDA mfupi uliopita, nimeonana na Mh. #TunduLissu katika chumba chake hospitali ya Nairobi na kuzungumza naye kuhusu hali yake na anavyoendelea.UKWELI ni kwamba, ameumizwa vibaya. Imeelezwa kwamba MADAKTARI wanaendelea na hatua kadhaa za matibabu, wakiwa wameanza kwa kumuimarisha (stabilization), ili kuufanya mwili uweze kumudu hatua zaidi za utibabu anazopaswa kufanyiwa. AIDHA, katika kuongea naye, Mh. Lissu ameonesha uso wa tabasamu, huku akimshukuru MUNGU kwa kumruhusu kuwepo hai. NAAMINI kwamba hatua zaidi na za haraka zitahitajika kumsaidia apate huduma za kitabibu katika ubora na ufanisi uliopo kwa sasa duniani. Ni maombi yangu kwetu SOTE , tuweke pembeni tofauti zetu za kiitikadi, ama mitazamo, tuungane na kushikamana kama Taifa kwa ajili ya kumwomba MUNGU anyooshe mkono wake, na kumponya. HALIKADHALIKA, SOTE tuungane kutoa msaada wa hali na mali kwa kadri ya uhitaji wake. AMANI iwe naye! 

Mengine yote aliyoyasema Nyalandu unaweza kuyafahamu kwa kubonyeza play hapa chini….

MSIKILIZE HAPA:

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com