Kwa Sasa Sina Mpango Wa Kuoa - Chege
Msanii wa muziki Bongo, Chege amedai kwa sasa bado hajafikiria mipango ya kufunga ndoa.

“Ni suala jema na ambalo linatakiwa lipewe nguvu na Mwenyenzi Mungu pamoja na juhudi zangu. Nikisema Mwenye Mungu ni kumpata mtu ambaye ni right choice kama mke ambaye nitaishi naye”. Kauli hiyo aliitoa Chege katika mahojiano na Bongo5 na kuendelea;

“Unajua kuoa ni kujifunga kabisa huyo ni wa milele ingawa inatokea bahati mbaya mtu unaweza ukaacha mwanamke lakini inabidi uchagua chaguo ambalo unaweza ukaishi nalo. Isiwe unaoa kwa sababu ya trending za watu, mimi siwezi kuoa kwa style hiyo,” amesema Chege.

Pia amesema kuwa familia yake hasa mama yake mzazi, kaka na ndugu wamekuwa wakimuuliza kuhusu jambo hilo na jibu lake siku zote limekuwa ni hilo hilo.

Chege kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Run Town’,  pamoja na ‘Najiuliza’ aliyowashirikisha Ray C na Sanaipei Tande.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com