Baada ya kusambaa kwa taarifa za Lady Jaydee kujitoa katika lebo kubwa Afrika ya Rockstar 4000 ambayo pia inamsimamia Alikiba na Ommy Dimpoz, mapya yaibuka.

Akiongea na Bongo5, mtu wa karibu wa msanii huyo, amesema Jide hajawahi kusaini mkataba na Rockstar ndio maana hakuna picha zilizowahi kuonyesha mkataba huo, alikuwa anafanya kazi na Seven Mosha ambaye ni bosi wa lebo hiyo kama rafiki yake wa muda mrefu ili kuweza kumsaidia kazi za muziki wake.

Nafikiria kaamua tu kuacha kufanya kazi na Seven, wewe mwenyewe unaona wasanii wote wa Rockstar au hata wa WCB au artist yoyote anaposaini contract huwa anaonyesha kwenye media na anakuwa anatangazwa kabisa kuwa ni msanii mfano kama wa Rockstar ni wa Rockstar. Kwa Jaydee hiko kilikuwa hakijafanyika ni kwamba walikuwa wanafanya kazi tu yeye na Seven na sio kwamba yeye alikuwa anafanya kazi na Rockstar direct,” kimesema chanzo hiko.

Pia ilikuwa in process kwamba wanapimana kuwa baadae Jaydee ataingia kwenye Rockstar lakini nafikiria haikufikia muafaka wa yeye kuingia may be. Nasema may be inaweza ikawa hawakufikia malengo ya pamoja kwamba artist anakuwa na malengo yake kwa meneja lakini hakufikisha au msanii hakufikisha malengo ya meneja ambayo alikuwa anayafikiria, hizo ni issue zote zinazowezekana,” kimeongeza.

Lakini ni watu ambao walikuwa wanafanya kazi tangu zamani, hata wakati ule Gardinani meneja wake lakini bado alikuwa anafanya kazi na Seven. Kama kulikuwa na kitu cha Jaydee ambacho anaweza kukipush alikuwa anafanya kwa sababu ni marafiki wa siku nyingi.”

Hata hivyo mtu huyo amesisitiza kuwa hakuna ugomvi wala tatizo lolote lililopo kati ya Jide na Seven kwani bado urafiki wao upo pale pale.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com