Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jioni hii na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya CHADEMA, Hemedi Ali kutoka Nairobi Kenya ambapo Tundu Lissu amelazwa zinasema kuwa kiongozi huyo ametolewa salama katika chumba cha upasuaji baada ya masaa 7 na kudai upasuaji umefanyika kwa mafanikio.

"Mh Tundu Lissu ametolewa salama katika chumba cha upasuaji baada ya Masaa 7 tangu saa nne asubuhi hadi sasa saa kumi na moja jioni na upasuaji umefanyika kwa mafanikio hivyo yupo 'Executive ICU' kwa uangalizi wa karibu zaidi. Na tunawahakikishia kuwa madaktari wametueleza hakuna tishio lolote kiafya yuko macho na fahamu zote na hii ndio ilikuwa hatua ngumu na Mungu ametupitisha hivyo tuendelee kumuombea apone haraka" aliandika Hemedi Ali

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com