Jumatatu kuanzia saa saba mchana Ndug Hamisa Mabeto atafunguka kupitia Clouds Fm kwenye kipindi cha XXL!Hii.imekuja baada ya mzazi mwenzie Diamond Platinumz kufunguka wazi na kueleza mengi kuhusu wao na kumkana hadharani japo alimkubali mtoto...
Moja ya mambo yaliyo mkera Hamisa ni kitendo cha Diamond kusema hawakuwa na ahadi yeyote ile wakati ukweli ni kwamba Diamond Platinumz alimuahidi kumuoa kabisa na ndio maana alikubali kutembea nae na anasema Diamond alisema anampenda yeye kuliko Zari!

Pamoja na hilo Hamisa anakuja kukanusha kuhusu mambo mengi aliyo yasema Diamond hasa ya kusema alikuwa anampa kila siku elfu 70+ na kumkubali mtoto toka mwanzo...jambo ambalo Hamisa anasema ni urongo...

Sasa anasema jumatatu atasema mengi na atasema kila kitu na kuhusu aliyekuwa ana record video zao na aliyekuwa ana husika kuzivujisha....

Wana jamvi naomba niishie hapa na tusubiri jumatatu saa 7 clouds Fm.

NB: Huu unaweza kuwa mwaka mbaya kwa Diamond maana Hamisa anakuja kumwaga mboga na kutoboa masufuria kabisa...
Wale ambao hampendi habari za Diamond na Zari nawashauri.msitumie Smart phone mpaka mwakani maana hii iliyobaki ni ya habari zao tuuu...

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com