Msanii wa muziki wa kizazi kipya Amber Lulu ambaye amejipatia umaarufu kwa kupiga picha za utupu na hatimaye kuingia kwenye muziki wa bongo fleva, amesema sasa hivi ana 'stress' za kazi zake hivyo hataki kuyapa nafasi mambo ambayo yatamuharibia.

 Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Amber Lulu amesema sasa hivi hataki mambo ya skendo ikiwemo kujibizana na 'video queen' mwenye sifa kama yake Amber Ruth, pamoja na matukio mabaya yatakayomuharibia kazi zake kama kuvuja kwa picha za utupu alizopiga na msanii Young Dee.
"Hivyo vitu siwezi kuviendekeza tena sasa hivi, nina 'stres' za kazi zangu. Nimetia pesa kwenye kazi sasa lazima niwe makini na masuala ya msingi", amesema Amber Lulu.

Amber Lulu hivi sasa ameamua kufanya muziki ambapo mpaka muda huu ana kazi mbili sokoni, ikiwemo 'watakoma' na 'Give it to me'.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com