Na Zawadi B Lupelo

Tulipokuwa tukisoma kiswahili mwalimu wetu wa fasihi (kiswahili 2) alipenda sana kutoa tafsiri ya neno mojamoja. Alituambia SANAA ni UFUNDI wa kueleza mawazo yaliyo katika fikra za mwanadamu. Ni kweli mwanadamu ana mawazo mengi sana lakini kuna namna ya kueleza hayo mawazo hivyo basi wanachokifanya wasanii ni ule ufundi wao wa kueleza yale yaliyomo akilini mwao. Kilichomo kwenye akili ya Diamond (mawazo yake) yanaweza yakawemo pia kwenye akili ya mtu mwingine yeyote lakini mtu huyo asiwe na ufundi wa kueleza mawazo hayo kama anavyofanya Diamond Platnumz. Anaweza asiwe na sauti kama yake, anaweza asiwe na uwezo wa kuandika mashairi kama yake, uwezo wa kunata na beat kucheza nk.
Maneno ya mwalimu wetu wa kiswahili 2 hayakuwa mbali na sheria zetu hasa inapokuja kwenye sanaa. Sheria za hati miliki zinatambua uwepo wa ufundi binafsi kwa msanii wa kuwasilisha mawazo aliyonayo ndiyo maana sheria inalinda ule ufundi wa msanii na si vinginevyo.
Ili nieleweke vyema tambueni kwamba katika sheria za hati miliki za wasanii (copyrights laws) kuna kitu kinaitwa ideas na kitu kinachoitwa expression of an idea, sheria haiprotect idea inaprotect expression ya ideas. Kiufupi naweza kusema expression of ideas ndiyo huo ufundi uliotumika lakini ideas ni mawazo. Kama nilivyoeleza hapo juu sometimes ideas (mawazo) yanaweza kufanana lakini hatutegemei ufundi wa kuyaeleza hayo mawazo kufanana.

Katika wimbo wa WCB "Zilipendwa" na ule wa Matonya "Zilipendwa" ukisikiliza kwa makini utagundua kilichomfanya Matonya alalamike ni baada ya kuona ideas za nyimbo hizo mbili zinafanana yaani ideas zao wote wawili ilikuwa ni kuelezea vitu na watu mbalimbali waliokuwa hot au wanafanya vizuri enzi hizo lakini sasa wamepitwa na wakati. Hiyo ndiyo idea ya hizo nyimbo mbili.

Kama nilivyosema awali kufanana ideas si kosa kwa sababu kuna wakati watu huwa na mawazo yanayofanana kuhusu jambo fulani na huenda siyo wao tu wenye ideas hizo wapo watu wengine wengi wenye ideas za namna hiyo lakini ukiwaambia express wataexpress kwa namna tofauti hapo ndipo linapokuja neno sanaa (ufundi wa kuwasilisha mawazo uliyonayo)

Kitu kingine ambacho kimemshtua Matonya ni neno "Zilipendwa", It is obvious kwamba sheria yetu ya hati miliki na siyo sisi tu bali dunia nzima haiprotect maneno, maneno yanakuwa protected kwenye trade marks na service marks mara nyingi majina ya kampuni na bidhaa lakini siyo katika muziki. Katika copyright laws huwezi ukawa na hati miliki ya neno na tukifanya hivyo maana yake maneno mengi sana itabidi yasitumike tena maana maneno zaidi ya asilimia 90 yameshaimbwa.

Sheria yetu ya Tanzania ya hati miliki inaitwa Copyright and Neighbouring rights Act ya mwaka 1999 kifungu cha 5(2)(d) inaeleza kwamba kitu kinachokuwa protected kwenye mziki ni Instrumental na Vocals tu na si neno au vinginevyo hii ni kwa sababu hapo ndipo penye ufundi. Ufundi wa mwanamuziki upo hapo kwenye Vocals na instrumentals na si kwenye maneno kama Matonya anavyotaka kutuaminisha. Msanii hagundui maneno la sivyo Matonya anataka kusema yeye ni muhenga aliyegundua neno " Zilipendwa "

Ni jukumu la Matonya kuthibitisha kama ameibiwa vocal au instrumental na WCB la sivyo hana haki yoyote ambayo imevunjwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com