Shilole Amwaga Chozi Kisa Barua Hii Aloandikiwa na Mtoto Wake
Mwimbaji wa Bongofleva Shilole kupitia Instagram yake ameelezea hisia zake juu ya kilichomtoa machoni baada ya kuisoma barua aliyoandikiwa na binti yake wa pili Rahma aliyoiandika kwa lugha ya Kiingereza.

Shilole baada ya kusoma barua hiyo aliamua kuandikia ujumbe ulioashiria hisia za furaha hadi kumtoa machozi akiamini kuwa amemkuza binti huyo kwa sababu ya umri aliokuwa nao hakudhani kama angeweza kuandika maneno yenye ujumbe mzito wa aina hiyo.

Shilole ameandika>>>>”Rahma binti yangu umeniliza na hii barua yako. Siamim km Mungu amenikuzia kiasi hiki mpk leo katoto kangu ka pili kananiandikia maneno mazito hivi. Nakupenda sn mwanangu wewe na dada yako ndio urithi wangu na furahayangu….Nikivurugwa hukoo na ya ulimwengu nikitud nyumban nyio ndio faraja yangu.

“Simkufuru Mungu kwa kuishi maisha ya shida niliyopitia, sisikitiki kwa kukosa elimu bora na kutimiza ndoto zangu nyingi nilizokuwa nazo nachojua MIPANGO YA MUNGU SIO KAMA YA MWANADAMU….Namshukuru kwa kila alichonipa, jina, umaarufu, rizki, marafiki na ndugu wa kweli lkn zaidi WATOTO wangu ambao kila iitwapo leo ndio mnanipa nguvu ya kuamka kupambana kuvumilia matusi vikwazo na kila vipingamizi. Nataka msome mtimize mdoto zenu nizeeke nikiona mnakuwa mabinti wa kuigwa na mumpendeze Mungu na wanadamu.

“KAMA KUNA JAMBO NINAJIVUNIA KULIFANYA SAHIHI DUNIANI NA SIJAWAHI LIJUTIA NI MIMI KUKUBALI KUWA MAMA. By the way ndugu zangu sijui kidhungu nimekielewa vizur.” – Shilole.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com