STAA wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa, anatamani kumfuata aliyekuwa staa wa Taarab, Mzee Yusuf kwa kuokoka kwani anahisi siku za kufa zimekaribia.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, Shamsa alisema kuwa, kila kukicha anajikuta anatamani kuokoka na kuacha kila kitu anachokifanya, abaki kusali tu kwani ana hofu sana ya Mungu, lakini hajui ataanzaje, ingawa anajitahidi. “Nimejaribu kusali sala tano kila siku.

Kuna wakati ninasahau lakini kuna siku ninasali zote, ninaamini taratibu nitakuwa kama Mzee Yusuf, ninamuomba sana Mungu,” alisema Shamsa.

Ungana nasi Facebook Like page yetu hapa chini

Weka Maoni Hapo Chini Kuhusu Habari Hii

Facebook Blogger Plugin by Celebrity Swaggz

Post a Comment

 
Top