Real Madrid  Watwaa Ubingwa wa Super Cup kwa Kuichakaza Barcelona 2-1
Klabu ya Real Madrid imetwaa ubingwa wa Super Cup wa nchini Hispania baada ya kuwagaragaza mahasimu wao, Barcelona kwa goli 2-0 kwenye mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu usiku wa kuamkia leo.
Real Madrid bila ya Cristiano Ronaldo aliyefungiwa mechi tano kwa kosa la kumsukuma mwamuzi kwenye mchezo wa awali, walianza kupata bao la kwanza lililowekwa kimiani na kinda wa mabingwa hao wa Ulaya, Marco Asensio kunako dakika ya 4 kabla ya Karim Benzema kutupia goli la pili la ushindi kunako dakika ya 39 kipindi cha kwanza na mpaka filimbi ya mwisho, Madrid 2 Barcelona 0.

Kwenye mchezo wa raundi ya kwanza, Real Madrid waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 ugenini kwenye dimba la Camp Nou mwishoni mwa wiki kwa goli la kujifunga la Gerald Pique, Cristiano Ronaldo na Marco Asensio huku bao la kufutia machozi kwa upande wa Barcelona likifungwa na Lionel Messi kwa mkwaju wa penati.

Real Madrid wametwaa ubingwa huo kwa jumla ya goli 5-1 dhidi ya Barcelona na kumfanya kocha Zinedine Zidane kuongeza idadi ya vikombe na kuweka rekodi ya kuwa kocha mwenye mataji mengi (7) kwa muda mfupi klabuni hapo .

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com