Ndoa ya Nuh Mziwanda na mkewe Nawal ilioyofungwa Novemba imeingiwa na kidudu mtu kilichopelekea ndoa hiyo kuvunjika licha ya kuwa imeweza kuleta tunda la Anyagile (Anya).

Akiongea katika U-Heard ya Clouds FM Jumatano hii, Nawal amethibitisha yeye na msanii huyo wa ‘Jike Shupa’ wameachana na kila mtu anaishi maisha yake kwa sasa na tayari yeye ameshafunga ndoa nyingine.

 “Sina mume mimi, Nuh wakati anaamua kurudi kwenye dini yake (Ukristo) hakunishirikisha na mimi sasa hivi nipo kwa bibi yangu Msasani, pia nimesha olewa na mtu mwingine,” amesema mrembo huyo.

Pia Nawal amedai kuwa ni kweli ameondoka kwake kutokana na Nuh kuwa mkosaji na mpaka sasa hamjali mtoto wao kwa chochote ila kama aliweza kumzaa basi anauwezo wa kumlea mtoto huyo.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com