MSANII wa filamu Bongo, Flora Mvungi amefunguka kuwa, madai ya kwamba yeye na mumewe Hamis Baba ‘H- Baba’ hawako pamoja yametokana na kila mmoja kubanwa na majukumu yake.
Akizungumza na Ijumaa, Flora ambaye kwa sasa anasomea mambo ya Uandishi wa Habari katika Chuo cha Royal kilichopo Ubungo jijini Dar alisema muda mwingi anautumia kusaka elimu na mambo yake binafsi hivyo kuwa mbali na H-Baba ambaye naye huwa jijini Mwanza kwa ishu za kisanii.

 “Wanasema eti nimeachana na H-Baba, siyo kweli ni majukumu tu, yeye yuko na mambo yake na mimi nina mambo yangu na hatushirikiani katika mambo ya sanaa ndiyo maana yanaibuka hayo. Ndoa yetu iko poa tu na niseme tu kwamba nampenda sana mume wangu,” alisema Flora ambaye ni mama wa watoto wawili.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com