Mrembo Sanchoka Aelezea Siri ya Umbo Lake Kumfunika Wema Sepetu.....
WIKI iliyopita ilikuwa ya kihistoria katika Shindano la Figa Bomba 2017 linaloendeshwa na gazeti hili baada ya kufika kilele na modo, Sanchoka ‘Sanchi’ kuibuka kidedea kwa kuwafunika wenzake wawili, Sasha pamoja na Wema Sepetu walioingia tatu bora.

Katika shindano hilo lililodumu takribani miezi miwili likijumuisha mastaa mbalimbali wenye figa matata Bongo zaidi ya 22, Sanchi aliweza kudhihirisha kuwa ni namba moja baada ya kupigiwa kura nyingi na mashabiki.

Leo katika kona hii, Sanchi anafunguka siri ya ushindi na jinsi alivyoweza kumfunika Wema kwa kalio.

Ijumaa: Unajisikiaje kuwa mshindi wa Ijumaa Figa Bomba 2017?
Sanchi: Najisikia vizuri nimeweza kuudhihirisha uzuri wangu kwa washiriki wote nilioshindana nao.
Ijumaa: Unajisikiaje kuwa mmoja wa wasichana warembo Bongo? Sanchi: Najisikia vizuri sana na uzuri umenifanya kujiamini popote ninapoenda. Ijumaa: Kutokana na umbo lako ni usumbufu gani unapata?
Sanchi: Unajua kuna kipindi mtu unatamani kukaa hata ndani siku nzima tu hata siku tatu kwa ajili ya kukwepa usumbufu.

Ijumaa: Picha zako mara nyingi zinaachaga viungo vyako wazi ni kwa nini?
Sanchi: Ni hobi yangu tu na najisikia furaha kufanya hivyo kwa sababu niko huru na kazi zangu.
Ijumaa: Kuna tetesi kuwa maisha yanaenda kutokana na umbo lako ni kweli?

Sanchi: Hakuna maisha yanayoenda ukiwa na umbo kwani watu wasiokuwa na maumbo maisha yao yanaendaje?
Ijumaa: Vipi una mpango wa kuzaa hivi karibuni?

Sanchi: Huo mpango upo mwakani nalifanyia kazi hilo suala.
Ijumaa: Unaweza kutuambia siri ya kumfunika Wema kwenye shindano la Figa Bomba?

Sanchi: Kikubwa ni kujiamini na kura za mashabiki kwenye shindano. Sijisifii sana lakini mashabiki ndiyo walioamua baada ya kuona umbo langu kuwa naweza kuwafunika hao watu.

STORI: IMELDA MTEMA

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com