Mercy Masika na Angel Bernard kuwapokea majeruhi Lucky Vincent
Msanii wa muziki wa injii kutoka nchini Kenya, Mercy Masika pamoja na Angel Bernard wanatarajiwa kuudhuria hafla ya kuwapokea watoto walioenda kutibia nchini Marekani ambao walinusurika katika ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent ya Arusha.Watoto hao Doreen Wilson na Sadia wanatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa hii Augost 18, 2017 ambapo watapokelewa katika uwanja wa ndege wa KIA, kilimanjaro.

“Shukrani wanamuziki wa injili Mercy Masika kutoka Nairobi (ikiwa ni mara yako ya kwanza kukanyaga ardhi ya Arusha) na Angel Bernard wa Arusha kwa kujitolea kwenu kushiriki baraka hizi za kuwapokea watoto wetu,” ujumbe huo ameuandika Mbunge wa Singida Kasikazini, Lazaro Nyalando na kuongeza

“Nimefurahia utayari I wenu, na shauku mliyonayo kuhusu hafla hii. Naamini wana familia, ndugu, jamaa na marafiki, ikiwa ni pamoja na viongozi wetu wote watafurahia sana vipawa vyenu katika kumtukuza Mungu. Watoto Doreen, Wilson na Sadia wataikumbuka siku kuu ya ujio wao kwenye nchi yao pendwa Tanzania wakiwa wameuona mkono wa Mkombozi katika maisha yao,”. ameandika katika Instagram.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com