Madee Yamemfika Hapa Aamua Kumuangukia Wolper
Rais wa Manzese, Madee amefunguka kwa kumuomba radhi msanii wa bongo movie Jacqueline Wolper kwa kitendo cha kumfanya katuni mrembo huyo katika video yake mpya ya wimbo 'Sikila' bila ya ridhaa yake mwenyewe.

Madee ameomba msamaha huo mbele ya kamera za eNewz kutokea EATV baada ya Wolper kudai anateenda kumshtaki kwa kitendo cha kumtumia katika kazi zake bila ya kuwa na makubaliano baina yao kwa kuwa ni kinyume na taratibu zake.

"Niliamua kumtumia Jacqueline Wolper baada ya 'director' kuniambia nitafugte picha ya msanii yeyote maarufu ndipo nikaamua kumpatia picha ya ya Wolper na kabla ya kumtumia nilimpigia simu, nikampa taarifa ili aelewe kinachoendelea", alisema Madee.
Pamoja na hayo, Madee amedai haamini kama ni kweli mrembo huyo anataka kumfungulia kesi juu ya jambo hilo.

Ungana nasi Facebook Like page yetu hapa chini

Weka Maoni Hapo Chini Kuhusu Habari Hii

Facebook Blogger Plugin by Celebrity Swaggz

Post a Comment

 
Top