Fid Q  Asema 'Zimbabwe' ya R.O.M.A Utakuwa Wimbo Mkubwa kwa Mwaka Huu
Rapa Fareed Kubanda 'Fid Q' amefunguka kuhusiana na wimbo mpya wa Roma Mkatoliki 'Zimbabwe' na kudai kuwa msanii huyo amejua kukamata hisia za mashabiki kwa kuimba ukweli uliyomtokea miezi michache iliyopita huku akimsifu ndivyo hip hop unavyotaka.

Fid Q amesema kuwa Zimbabwe ni wimbo uliyokuja kufanya mapinduzi makubwa kwenye 'industry' ya hip hop kwa mwaka 2017 pia kuutaja kuwa huwenda ukawa ndiyo wimbo mkubwa kwa mwaka huu.

"Roma kajua kuteka hisia za mashabiki zake, Zimbabwe ni wimbo mkubwa sana kuwahi kutokea mwaka huu ukizingatia. Umevunja rekodi ndani ya siku moja kwenye Youtube. Alichokifanya Roma ndicho hip hop inachotaka, hakuna mtu ambaye alikuwa hajui kama Roma katekwa na watu walikuwa wakimsubiri kuona anarudi vipi kwa hiyo nampongeza kwa kuwa amezingatia kiu ya mashabiki zake", alisema Fid Q.

Kwa upande mwingine, Fid Q amewataka wasanii kufanya kazi zilizokuwa na ubora na zitazoishi muda mrefu na siyo kukimbilia kolabo za kimataifa ambazo hazitawasaidia kufika mbali kama jinsi wanavyotaka.
Kwa sasa Fid Q anatamba na ngoma mbili alizoziacha ambazo ni 'Ulimi mbili pamoja Fresh'

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com