Dulla Makabila Adata na Penzi la Bongo Movie
Msanii wa Singeli nchini Tanzania, Dullah Makabila anatarajia kufunga pingu za maisha na Husna Sajent ambaye ni muigizaji wa bongo movie hivi karibuni huku baadhi ya watu wakimshangaa Makabila kuamua uamuzi wa kutakumuoa mwanamke aliyemzidi umri.


Mipango hiyo ya Harusi ya Dullah imewekwa wazi na meneja wa Snura HK wakati akizungumza katika kipindi  cha eNewz kutoka EATV na kusema yeye kama mshenga anatamani kuona ndoa anayounganisha iweze kuleta matunda mazuri ya ndoa kwa kuzaa angalau watoto wawili na kuendelea.

"Kwa sasa nategemea kusimamia ndoa ya Bi. Husna na Dulla Makabila ambao wamekuwa katika mapenzi kwa muda mrefu sasa, natumaini ndoa yao itadumu kwa muda marefu tofauti na ilivyokuwa ndoa ya Nuh Mziwanda kwa kuwa ni watu wazima na wanapendana kweli", alisema HK.

Pamoja na hayo, HK amesema ameshangazwa sana kitendo cha kuvunjika ndoa ya Nuh Mziwanda ambayo yeye ndiyo alikuwa mshenga wake japo hakutaka kuweka wazi sababu ya kuvunjika kwa ndoa hiyo.

Kwa upande mwingine, HK amesema kilichotokea kwa Nuh Mziwanda hapendi kukiona tena kikiwatokea Dullah Makabila na mke wake mtarajiwa.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com