Maisha ni zaidi ya kuishi,maisha ni mahusiano na katika hili basi maisha yana maana zaidi ya kuishi.Mfano pale unapo amka asubuhi na kugundua kuwa kuna binadamu kama wewe wanaishi katika dunia hiyo hiyo ambayo na wewe unaishi,inakupa mawazo ya kufanya mipango ya maisha,kama vile kufanya biashara,kutoa huduma au kupokea huduma,moja kwa moja kutoka kwa binadamu wenzako.

Hii ina maana kwamba hata uwe mbinafsi vipi,huta tamani kuishi peke yako duniani,hii inatupa picha kwamba binadamu wenzetu ni wa muhimu zaidi katika kutimiza maisha yetu ya kila siku,hivyo ningeanza kwa kusema maisha ni mahusiano kati ya binadamu na binadamu.


 DIAMOND PLATNUMZ

Umekuwa ukipigania maisha yako ya kila iitwayo leo,naamini unatamani kesho iwe tofauti na leo,uzidi kuimalika katika mapambano yako ya kupata riziki.

Ulipo anzia sipo ulipo sasa,ulisha wahi kujiuliza ulifikaje hapo?Je ni juhudi zako binafsi (wewe kama wewe).Au ni juhudi za maisha yako (wewe na binadamu wenzako),mi naamini ni vigumu kufanikisha lolote katika hii dunia pasipo na maisha ya binadamu wengine.

Hivyo tukubaliane kwanza kwamba umefika hapo sababu ya binadamu wenzako ambao ulishirikiana nao ndiyo maana ukafika hapo.Pasinge kuwa na binadamu usinge kuwa hapo ulipo,maana ungemwimbia nani,ungeshauriwa na nani,ungeonyesha uwezo wako kwa nani,nani angekutengenezea nyimbo,nani angetizama video zako,hivyo ujue umefika hapo sababu ya watu wote unao wachukia au kuwapenda,kila binadamu huwa na mchango kwa binadamu mwingine moja kwa moja au kinyume chake.

Utajiri,Fadhira na chuki dhidi yako

Kwa bahati mbaya hakuna maskini anayetajirika akakosa timu ya wadai fadhira,sababu utajiri wa maskini hua na mnyororo wa wafanikishaji hadi kufikia utajiri huo,fahamu kuwa utajiri wa maskini una madeni ya fadhira kuliko utajiri wa tajiri,kama nilivyo sema binadamu ndiyo kakufikisha hapo.

Ushauri wa namna ya kurejesha fadhira

Watambue wadeni wa mafanikio yako,na hakikisha huwapotezi katika orodha na kumbukumbu zako,fahamu namna ya kuwalipa wadeni wako wa fadhira na uwalipe haraka.

Ukweli ni kwamba huwezi kuwalipa wadeni wako wa fadhira kwa pesa,au thamani sababu ukifanya hivyo ni sawa na kulipa fadhira,fadhira hailipwi fadhira inarejeshwa,naamini si kwamba waliokusababisha wewe kufika hapo walikuwa wanatoa pesa zao mifukoni na kukupa la hasha inawezekana walitumia muda wa maisha yao hata kama dakika moja kwa ajili yako kutoa hatua ya ngazi hata kama moja ila moja kwenda juu.Watu hawa naamini wanacho hitaji kikubwa kutoka kwako ni HESHIMA na KUTAMBULIKA.

Naamini hata wewe hapo ulipo umelifanyia taifa letu la Tanzania vitu vikubwa kwa kulitambulisha mahali pengi duniani kupitia sanaa ya muziki,naamini kitu kikubwa ambacho unatarajia kutoka katika taifa lako kutokana na kazi hiyo ni HESHIMA na KUKUTAMBUA.Lakini je? Wewe,umeyafanya hayo kwa wale walio kutambulisha Tanzania?

Haijalishi amekuchangia nini,iwe muda wa maisha yake,ushauri wake au vitendo vyake,ambavyo kwa namna moja au nyingine vilisababisha wewe kupiga hatua ya mbele zaidi,yakupasa KUMTAMBUA na KUMHESHIMU,awe mdogo au mkubwa.

Swala la mali na pesa hiyo ni zawadi yako na si lazima kumpa mtu,kama ikitokea mdai fadhira anadai pesa au mali,huyo hakuwa anakusaidia au kukupa fadhira huyo alikuwa anakukopesha fadhira au kukuajiri achana nae.

Chuki dhidi yako

1.Sababu za chuki

*Hujajua namna ya kufurahia mafanikio yako kulingana na jamii unayo ishi nayo.

Nasibu unayakumbuka maisha yako ya Tandale?Maisha ambayo mama yako alikuwa anapigania mpate mlo wa siku?Maisha hayo bado yapo kwa watanzania wengi hadi sasa.

Hivi unajua uliwezaje kupata ridhiki kubwa ambayo inakuhakikishia kupata chakula bila tabu leo hii?Je,uliipata kwa maonyesho ya majivuno ya starehe,na maonyesho ya thamani za mali na vidani vya gharama?

Au uliipata hiyo ridhiki kwa kuheshimu kila uliyemuona atakupa njia,ya kufika hapo ulipo?Kwa hiyo njia uliyo itumia zamani unadhani imepitwa na wakati,ukadhani njia ya majivuno ya mali,starehe na vidani kwa walio kupa mtaji itakusaidia kukubeba zaidi ya pale walipo kufikisha?HAPANA!

Fahamu kwamba wewe ni kioo cha jamii,kioo cha watu ambao wengi ni maskini na wachache matajiri,hivyo watu watapenda kukutazama kama mtu unaye wajali na kuwathamini kwa kile ulicha jaaliwa kukipata,mimi naamini unaweza ukaonekana kwa jamii katika mtizamo tofauti zaidi ya kwamba Diamond Platnumz ni mtu mwenye majivunoya mali na mbwembwe za starehe sababu njia hiyo itakujengea watu wenye chuki hata bila sababu.

*Sababu nyingine ya chuki ni kwamba Diamond Platnumz hutambui thamani yako,kwa hatua uliyo fikia,ulipaswa kujiamini na kuwa na busara ya hali ya juu kabisa.

Hatua uliyofikia kimziki,ni ya kuheshimiwa,Hukupaswa kabisa kwa level zako kuonyesha chuki dhidi ya wasanii wengine, kwa nini usiache chuki hizo zibebwe na kushugulikiwa na mashabiki,na siyo kujiingiza wewe na brand yako.

2.Ushauri

*Jaribu kutumia muda mwingi katika kuonyesha matukio ya kijamii zaidi,kupiga picha na mashabiki zako,kuonyesha picha za matukio ya “charity” mbalimbali unazo zifanya,picha ambazo zitaonyesha uko jirani zaidi na jamii,pia picha za familia yako,zitakufanya uonekane hushangai mafanikio na utaonekana huna ushindani na waliokupa riziki,bali utakuwa ni mtu wa jamii tena mtu wa watu,naamini haita kupunguzia kitu ila itakujenga na kukupa thamani zaidi.

Mfumo wa maonyesho ya vidani na thamani pamoja na maisha ya starehe,hayavutii kwa jamii yetu hii ambayo wewe umetoka nayo,huo ni utaratibu wa Kimagharibi,na siyo kwetu huku.

Jifunze kwa matajiri wakubwa hata hapa Tanzania wanapesa lakini mitandao yao ya kijamii wameitumia katika sura ya kuwa wao ni sehemu ya jamii na wako nayo pamoja katika shida na raha.

* Fahamu kwamba brand yako ni pesa nyingi sana,unachokifanya chochote ni pesa kwa wengine kama isipo kuwa kwako.

Acha kurudia vidato na hilihali ulifaulu vizuri tena sikunyingi,unacho tafuta ni nini?Kwani huko kwenye level zako hakuna mitihani ya juu hadi uanze kurudia vidato,hivi unadhani ikitokea umeenda kufanya mtihani wa kidato cha chini na wewe kidato cha juu,harafu ikatokea ukapitwa na mwanzafunzi wa chini unadhani kitakacho fata ni nini kama siyo aibu na kuzomewa?

Ushindani na mtu uliyemzidi huleta dharau na kuvunja heshima,

Mara nyingine ufahamu kazi yenu hii ni sawa na mchezo wa mpira,kama wewe beki mshambuliaji anaweza akakuchokoza makusudi ili ufanye faulo watu wapige penati,na ubaya kombe hua halibagui mshindi,yoyote aliyeshinda anaondoka nalo.

MAMBO 10 YA KUZINGATIA WEWE DIAMOND PLATNUMZ

1- Epuka kuongele maisha yako kwa watu,ambao huwafahamu vizuri hasa marafiki wapya wa muda mfupi,huwezi jua nani kaja kukupeleleza.

2- Epuka kujenga urafiki wa dhati na uaminifu kwa wanasiasa (urafiki wako uwe wa malengo kama wa kwao ulivyo wa malengo,wakati wote kuwa makini).

3- Kuwa makini unapotaka kurejesha urafiki na mtu uliyegombana nae,inawezekana hakumaliza hasira anaweza akawa anakuja kuleta jipya.

4-Kuwa makini na watu wako wa jirani,marafiki,ndugu,wafanyakazi wenzako inawezekana mnacheka pamoja na kuonyeshana uaminifu,ila msaliti yu kati yenu,usipende kufahamika sana hata kwa wanao kuhusu sana.

5-Usipende kutoa matamko au kujibu hoja kama hakuna ulazima.

6-Siku zote fahamu wewe ni kioo cha jamii,na jamii lazima ijione ikikutizama isije ikawa inaona mtu wa bandia.

7-Fahamu kwamba chuki unazo pata ni mtaji wa mafanikio yako,zinakuja ili kukuboresha kukupa hasira ili ufanye kazi na kukua zaidi,walio fanikiwa duniani ndiyo wenye bahati ya kuchukiwa na ndiyo maana huzidi kufanikiwa sababu,chuki ni mbolea tosha ya mafanikio,ukiona huchukiwi ujue umesha fikia hatua ya Mr. Nice kwani wakikumaliza hawatahangaika na wewe tena watahamia kwa mwingine,kadri unavyo fanikiwa ndivyo kasi ya chuki huongezeka.

8-Fahamu kuwa una marafiki wengi sababu una pesa na una maadui wengi sababu unapesa,ukikosa pesa marafiki na maadui watakukimbia,hivyo kama unapenda pesa basi kuwa tayari kwa hayo.

9-Toa misaada kwa wahitaji,hasa watoto,kinamama na waremavu.

10-Usimwamini mtu hata kama ni dugu yako.

KIKUBWA NACHO KUTABILIA KWA MUJIBU WA SAIKOLOJIA NI KWAMBA UGOMVI USIYO NA SABABU HUISHA BIRA SABABU,NA HUYO UNAYEGOMBANA NAYE LEO BILA SABABU NI RAFIKI YAKO KESHO TENA BILA SABABU.

ILA KWA BAHATI MBAYA KUPITIA UGOMVI HUU USIO NA SABABU UMEZAA MAADUI WENYE SABABU NA HUENDA HAMTA KUJA KUWA MARAFIKI MILELE NA HAWA WAGOMVI WENYE SABABU.

By Jmaiko

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com