Amba Lulu Akili Kujichubua na Awatolea Povu Wanaomsema
Video queen aliyeikacha fani yake na kuzamia kwenye muziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu amekiri kuwa anajichubua rangi ya ngozi yake na kuwatolea mapovu wanaomsemasema kuhusu ishu hiyo.
Staa huyo anayetamba na ngoma yake ya Watakoma, aliyomshirikisha mkali wa Hip Hop Bongo, Country Boy, amewatolea mapovu watu wenye tabia ya kuchukua picha zake za miaka ya nyuma na kuzifananisha na za sasa, kisha kumsema kuwa anajichubua.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, amejibu mapigo kama ifuatavyo:
“Pale unapoona watu mapovu kibao ooh mweusi sasa na wewe si ujichubue. Au huna hela za kiduka cha usiku? Maisha ni mafupi sana.
“Mimi na feki, sasa mbona mnani-follow mna-like tena kuiga ndo msiseme, muulize tu Amber unatumia mkorogo gani, maana sio kwa mabadiliko hayo.
amber lulu

“Mimi napambana na tube zangu, pambana tu na wewe na hali yako. Kujichubua nijichubue mimi hasira upate wewe duh! Unazionea huruma pesa zangu wakati natafuta kwa jasho langu, kivipi.

“Na mwisho wake haimhusu mtu ngozi yangu pesa yangu mikono yangu naupaka vizuri maisha yangu.
Na hizo TBT ni za kitoto hapo nimekuwa mtu kabisa ngoja niwape kiboko kabisa sasa.

“Siogopi kwa sababu ndiyo mimi ndipo nilipotokea na ndivyo nilivyo kuwa wewe.
Tena sasa hivi nataka wa Kiarabu niwe Mhindi kabisa Waarabu nicheki Dm nizidi mie,” ameandika Amber Lulu.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com