Nandy.

KATIKA pasipoti yake ya kusafiria anatambulika kwa jina la Faustina Charles lakini kwa mashabiki wa Muziki wa Bongo Fleva wanamtambua kama Nandy a.k.a African Princess.
Anafanya poa katika Muziki wa Bongo Fleva kwa sasa ambapo ukiongelea miongoni mwa wasanii wa kike waliopo kwenye chati kwa sasa huwezi kumuacha. Ngoma iliyomtambulisha ilikuwa ni Nagusa Gusa ambayo remix yake amemshirikisha Mr.Blue.
Over Ze Weekend limekuwekea kwa ufupi baadhi ya mambo usiyoyajua kuhusiana na Nandy anayebamba kwa sasa na Ngoma ya Wasikudanganye.
Alikataa kuishi Nigeria
Alikuwa mshindi wa kwanza katika Shindano la Karaoke Barani Afrika la Tecno Own The Stage lililofanyika Februari 2016 nchini Nigeria.
Katika shindano hilo, Nandy aliibuka nafasi ya pili na kujizolea shilingi milioni 36 pia kuahidiwa kuingia katika lebo kubwa nchini Nigeria ya Chocolate City na kufanya kazi huko lakini alikataa na kujiunga na Jumba la Vipaji (THT) ambao yupo nao hadi sasa.
Nandy.
Anawavalisha mastaa
Nje ya muziki, Nandy ni bonge dizaina kwa mastaa…mavazi yake yote anayoonekana amevaa ya asili huwa anabuni mwenyewe na kushona.
Miongoni mwa watu maarufu aliowahi kula shavu la kuwa-bunia baadhi ya mavazi hayo ni Naibu Spika Dk. Tulia Ackson.
Milioni 36 zamtoa
Kati ya vitu anavyojivunia kupitia kipaji chake ni pale alipokuwa mshindi wa pili katika shindano hilo la Karaoke na kujipatia shilingi milioni 36 ambazo nusu yake zilimuwezesha kumiliki kampuni yake mwenyewe ya kubuni na kutengeneza mavazi ya asili na magauni ya harusi iitwayo Nandy African Print.
Ilikuwa atoke kwa Akili the Brain?
Kipaji chake kilikuwa kitoke kwa mara ya kwanza Akili Records chini ya Akili The Brain. Nandy anasema kuwa katika kuhangaika kwake kutoka kimuziki alishawahi kufika kwenye studio yake na kutengeneza ngoma nne lakini hazikufanikiwa kutoka mpaka alipopata shavu la kwenda Nigeria kwenye Karaoke ya Tecno.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com