Baada ya tetesi kuwa Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz ameiba wimbo wa Cheche kutoka kwa Msanii mchanga ajulikanaye kwa jina la Modala, Hatimae Ommy Dimpoz amejibu tuhuma hizo kwa kusema wimbo wa Cheche ni wake huku akiweka wazi kuwa amenunua mashairi ya wimbo huo kutoka kwa Mtunzi/Muandaaji wa muziki Lolipop.


Ommy Dimpoz amesema alinunua Wimbo huo kutoka kwa Lolipop mwaka jana ingawaje amechelewa kuuachia kutokana na muingilio wa ratiba lakini hakuwahi kuusikia wimbo wa Cheche wa Modala na hata wakati ananunua wimbo huo alimuamini Lolipop kwani ni mtunzi mzuri wa nyimbo na hakuambiwa kwamba wimbo huo tayari ulikuwa umenunuliwa.

“Mimi naamini Lolipop ni mwandishi mzuri pengine kuliko mimi…Kwahiyo mimi nina haki na wimbo wa Cheche na nilinunua kutoka kwake kwasababu ni mwandishi ambaye amewaandikia Wasanii wengi nyimbo.. Mimi nimewekwa mtu kati, kati ya Lolipop na Abby Dady lakini watu wajue wimbo huu ni wangu soo hata mkitukana tukaneni ila nasimama kwenye haki yangu wimbo wa Cheche ni wangu”,amesema Ommy Dimpoz kwenye mahojiano yake na Times FM.

Ommy Dimpoz amesema kama angekuwa ni yeye amesharekodi wimbo huo halafu anakuja kusikia kuna Msanii mwingine ameachiwa wimbo alioununua basi angeenda moja kwa moja kwa mtu aliyemuuzia na kumtaka amrudishie pesa yake badala ya kulalamika kuibiwa.

“Ningekuwa matatizo haya yametokea kwangu kuwa nimewapa pesa halafu nasikia wimbo wangu umeachiwa na msanii mwingine mimi ningemfuata Lolipop anirudishie hela yangu nisingeachia wimbo“,amesema Ommy Dimpoz.

Hata hivyo Ommy Dimpoz amesema kama kuna mtu anaona kaibiwa wimbo huo basi atafute haki yake ila anachojua yeye wimbo wa Cheche ni wake pia amewaomba Mashabiki waendelee kumpa sapoti kwenye kazi zake huku akiwataka waache matusi mitandaoni kwani sio ustaarabu.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com