Msanii wa hip hop Bongo, Young Killer ametoa sababu ya kusema hana hela katika diss track ‘True Boya’ aliyoiachia kwa ajili ya Nay wa Mitego.

Rapper huyo ameeleza kuwa aliamini baada ya kumjibu Nay kupitia ngoma hiyo ni lazima angekimbilia upande kujimudi kiuchumi ambapo amemzidi.

“Nimesema sina hela kwa sababu ujue tunazidia, na Nay ni mtu ambaye kiuhalisia anaonekana kanizidi vitu vingi kuhusiana na uchumi, kwa hiyo niliamni kabisa point yake kubwa itakuja umenijibu, lakini wewe huna hela ya kunizidi, kwa hiyo ile ilikuwa ni kwake, hana kingine cha kunizidi,” ameiambia Ladha 3600 ya E FM na kuongeza.

“Nataka tuje kimichano, tupeane kimichano, toa facts nitoe facts, toa point Young Killer muziki wako unaharibika kwa sababu ya hivi na hivi na mimi nitoe facts za wewe kuporomoka kimuziki,” amesema Young Killer.

Wasanii hawa wamekuwa na mvutano mara baada ya Nay wa Mitego kumchana na Young Killer katika ngoma yake ‘Moto’ lakini alikuja kujibiwa kutipitia ngoma ya True Boya.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com