Msanii Ommy Dimpoz ambaye sasa anatamba na ngoma yake mpya 'Cheche' amefunguka na kuweka wazi tuhuma za yeye kuiba wimbo na kusema hausiki hata kidogo kwani wimbo huo mpya aliandikiwa na kufanyiwa kila kitu na Goodluck Gozbert (Lollipop).

Ommy Dimpoz amesema hayo jana kupitia Friday Night Live (FNL) na kusema yeye hapaswi kuhusishwa hata kidogo kwani yeye alifuata utaratibu wote na kupata wimbo huo hivyo mtayarishaji wa muziki Aby Dad pamoja na msanii wake wanapaswa kudeal na Goodluck Gozbert (Lollipop) na si yeye kwani yeye ataendelea kuipa nguvu kazi hiyo sababu tayari ameshawekeza.

"Lollipop alisikilizisha chorus hiyo ya Cheche nikaipenda ila akaniambia wimbo huu haujakamilika, baada ya hapo aliutengeneza wimbo ule mwanzo mwisho kwa kuweka sauti zake mimi nilichofanya ni kufuatisha kile ambacho yeye amefanya, sijaandika chochote, wala kutunga melody wala chochote kile" alisema Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz aliendelea kusimulia kuwa
"Sasa baada ya wimbo kutoka baada ya mwaka mmoja kijana ndiyo ananiambia kuwa wimbo wa kwake, mimi ikabidi nimuulize Lollipop inakuaje hii akasema yeye alikwenda studio ya Aby Dad kufanya kazi zingine anadai baadaye akatengeneza kiitikio hicho na kuingiza sauti lakini Aby Dad akasema amependa kiitikio hicho atumie msanii wake, sababu yeye Lollipop haimbi nyimbo za hivi yeye anaimba nyimbo za dini tu, ila naomba hili nisiliongelee sana kwa sababu Lollipop mweyewe yupo naomba mumtafute ili aweze kuongea mwenyewe" alisisitiza Ommy Dimpoz

Mbali na hilo Ommy Dimpoz anasema yeye hakuna anayemlaumu hata mmoja kati yao
"Mimi sijui nini kimetokea kati ya hao watu wawili AbyDad pamoja na Lollipop lakini pia mimi simlaumu yoyote kati yao ila nachoomba tu wao wasinihusishe kwenye mambo yao waniache mimi niendelee na mambo yangu, sababu siwezi kurudi nyuma nishawekeza kwenye wimbo huu" alisema Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz ambaye sasa yupo chini ya usimamizi wa Rock Star4000 ameahidi wiki ijayo video ya wimbo huo 'Cheche' ndiyo itatoka rasmi.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com