`Msanii wa Bongo Flava, Ommy Dimpoz amekana madai ya kutaka kutumia jina la Simba na kusema majina ya wanyama yalimpitia mbali.

Kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM, Ommy Dimpoz ameulizwa kwanini katika moja ya picha alizopost Instagram akiwa na Mwana FA aliandika, ‘THIS IS SIMBA’.

Katika majibu yake Ommy Dimpoz amesema, “no sikusema am Simba, THIS IS SIMBA ni msemo unaotumika na mashabiki wa Simba Sport Club, kama umeona Msemaji wetu Haji Manara anapendaga kutumia THIS IS SIMBA.

“Siku ile tulikuwa tumetoka kwenye futari ya Simba tulikuwa tumealikwa, kwa hiyo tulivyotoka tukapiga picha nilivyofika nikapost ile, kwa sababu hiyo nikakumbusha tulitoka kwenye futari ya Simba na hata ukiangalia mashabiki wengi wa Simba walikujua ku-comment,” amesema Ommy Dimpoz.

Muimbaji huyo ameongeza kuwa huwezi kumuaminisha mtu kile  unachoamini wewe na hata ikitokea akahitaji kutumia jina la mnyama hatotumia la Simba kwa sababu wanyama wapo wengi.

“Kiukweli mimi majina ya wanyama yalinipitia mbali, kwa hiyo napenda kujiita hivi hivi Ommy Dimpoz nimeridhika nalo, na hata nikiamua kujipa jina la mnyama kuna wanyama wengi why nichague Simba, kuna Nyati kuna Swala, kuna Kasuku yote hayo unaweza ukaamua kwa nini hufuate jina moja huo utakuwa ukorofi,” amesisitiza.

Imekuwa ni kawaida kwa wasanii wa Bongo Flava kujipa majina ya wanyama, Diamond Platnumz anatumia jina la Simba, Dudu Baya anatumia jina la Mamba ambalo kipindi cha nyuma lilileta mvutano kati yake na Shetta baada ya kuanza kulitumia.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com