Siku chache baada ya kubainika kuwa, Miss Tanzania 2006-07 ambaye pia anatisha katika tasnia ya filamu nchini, Wema Isaak Sepetu ni mtumiaji mzuri wa nyama ya Nguruwe ‘Kitimoto’, imeonekana kuwa msosi huo umeanza kumharibu kwa kutokwa na minyama uzembe.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, kwasasa mrembo huyo ameongozeka unene na kuwa na ‘shavu dodo’ tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma kidogo, huku utumiaji wa nyama hiyo ukitajwa kama chanzo.

Akiongea na Mwandishi Wetu, rafiki wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa, ulaji wa Kitimoto kwa Wema huenda ukamuathiri kwani kwa muda mfupi ‘figa’ yake imeanza kubadilika.

“Yaani Wema kwa Kitimoto usimpimie kabisa, lakini sasa ulaji wa nyama hiyo umeanza kuuharibu mwili wake kwani katoka minyama uzembe, nimekuwa nikimshauri ale kwa kiasi lakini mwenyewe anaona sio ishu,”alisema shoga huyo wa karibu na Wema.

Katika siku za hivi karibuni, Wema alinaswa akipata nyama ya Kitimoto pamoja na ndizi za kuchoma katika baa moja bubu iliyopo nyuma ya Ukumbi wa Africentre uliopo Ilala jijini Dar es Salaam huku akishushia na kinywaji murua kisicho na kilevi.


Msanii wa filamu ambaye anajulikana zaidi kwa ‘taito’ ya Pacha wa Uwoya, Jacqueline Wolper amepigwa chini kwenye shindano la kusakata muziki, maarufu kama Serebuka.

Za chini chini zinadai kuwa, Pacha wa Uwoya ameburuzwa out ya mashindano hayo yanayosindikizwa hewani na runinga ya TBC1 baada kuwa mtoro kwenye mazoezi.

Aliposakwa kwa simu na kijiwe hiki, Jack hakupatikana hata.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com