Msanii wa Bongo Fleva, Ray C amedai kwa sasa hayupo katika mahusiano ya kimapenzi na mtu yeyote.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ‘Unanimaliza’, ameiambia FNL ya EATV kwa sasa hana muda kuwa na mtu zaidi ya kufanya kazi zake binafsi.

“Mimi hapana sipo kwenye mahusiano na mtu yeyote, kwa muda niliopoteza, hakuna tena muda wa kupoteza wa kumpa tena mtu mwingine naona kama muda umenipita sana, kwa hiyo akili yangu ipo kwenye kazi. Sioni kama ninaweza nikashare muda wangu na mtu mwingine, sina hata hizo feeling kwa bahati mbaya sana,” amesema Ray C.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com