Mkali wa wimbo ‘Dozee’ Nedy Music kutoka label ya PKP ya Ommy Dimpoz amefunguka kuwaweka sawa baadhi ya mashabiki wake ambao amedai hawajaelewa kauli aliyoitoa Ommy Dimpoz kuwa anatafutiwa management nyingine ya kusimamia kazi zake za kimuziki.
Dedy amedai kwa sasa bado yeye ni msanii wa PKP na muziki na ishu ya yeye kutafutiwa menejimenti mashabiki wameielewa vibaya.

“Watu walishindwa labda kujua nini alichokiongea nikiwa na maana kujua tafsiri ya neno lake kwasababu mswahili unaweza ukamuelekeza kitu yeye akatafsiri kivyake lakini yupo ambaye utamuelekeza kitu akajua maana yake maana yake ni kwamba kama itatokea Records Label kubwa kama aliyokuwepo yeye kwamba ikataka kufanya kazi kwasababu si tunafanya kazi na biashara kwahiyo kama kutakuwa na makubaliano ya kufanya kazi ya na biashara basi kutakuwa na utayari wa hivyo lakini si kwamba eti sasa hivi Nedy hayupo kwenye uongozi kwamba yupo ‘Yatima’ sio kweli,”

Jumatano iliyopita kupitia Clouds fm Boss wa PKP Ommy Dimpoz alisema “Ni vitu muhimu sana msanii kuwa na menejimenti, hata Nedy nimemtengenezea timu ambayo itakuwa inamsimamia mambo yake, kwa hiyo mimi sina he deck hivyo tunasimamia biashara yetu ya PKP kwa sababu tumewekeza pale, hakuna kilichoharibika, Kanye West alikuwa chini ya Jay Z lakini ana Good Music,”

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com