Tukio hilo lilifanyika jana Alhamisi ambapo A.Y alimvalisha pete mrembo huyo ambaye ni raia wa Rwanda na amekuwa naye katika mahusiano tangu mwaka 2008.

Kwa mara ya kwanza AY alimtambulisha mpenzi wake huyo Desemba mwaka jana wakati wa siku ya kuzaliwa ‘birthday’ ya mrembo huyo.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu wa karibu na wawili hao. Kwa kitendo hicho tunatarajia kuiona ndoa ya A.Y na mpenzi wake huyo siku chache zijazo akiwafuata mastaa wengine kama MwanaFA, R.O.M.A, Prof, Jay ambao wamefunga ndoa na wana-enjoy maisha ya familia.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com