STAA kutoka Bongo Muvi, Aunt Ezekiel ameweka wazi kuwa wazo la kushika ujauzito hivi karibuni halipo na kwamba kuzaa tena labda mpaka mwaka 2027 ambapo mtoto wake, Cookie atakuwa amefikisha miaka 10.

Akizungumza na Star Mix, Aunt alisema kuwa maisha ya sasa yamebadilika sana ni lazima hata kwenye kuzaa mtu ujipange ili kutoa nafasi nzuri kwa watoto kuweza kusoma na kuishi maisha bora kuliko kuwatesa.

“Jambo la kuzaa sasa hivi hapana kabisa labda miaka kumi ijayo kwa kuwa maisha yamebadilika sana jamani sio rahisi kama ilivyokuwa huko nyuma maana hata watoto watano ningezaa,” alisema Aunt.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com