Mtayarishaji na Mwanamuziki kutoka kundi la 'Navy Kenzo' Nahreel, amefunguka na kusema yeye na msanii mwenzake wa kundi hilo (Aika) katu hawawezi kupumzika kufanya muziki ili kusimamia wasanii waliopo chini yao kwani watakuwa wamerudi nyuma sana.

Nahreel ametoa kauli hiyo mapema wiki hii wakati akizungumza na EATV kupitia kipindi cha 5Selekt na kusema kwamba kupumzika kwao kwenye 'game' itakuwa ni njia ya kujipoteza wenyewe.

"Chini ya lebo ya The Industry kuna watu wengi nyuma, kama maprodyuza wapo wengine wawili ambao nasaidiana nao. Mimi na Aika hatuwezi kuacha kuimba kwa sababu tunasimamia wasanii, tutaendelea kuimba, kutengeneza nyimbo lakini kuwasimamia wasanii ambao tunaona wanauwezo mkubwa kuliko hata mimi au watu wakaribu waliotuzunguka" Nahreel.

Akizungumza kuhusu kutengeneza tu nyimbo za wasanii wa waliopo chini cha lebo yake kuliko wasanii wa nje, Nahreel amesema "Sisi tunafanya kazi na wasanii wote, hii siyo studio ya 'The Industry' tu. Lakini kuna utaratibu lazima ufuatwe. Wakifuata utaratibu ambao tumeuweka basi kazi za nje nyingi zitasikika. Tangu kuanza kwa mwaka 2017 kuna utaratibu wa kurekodi niliweka lakini wasanii wengi waliondoka kukwepa huo utaratibu" Nahreel aliongeza.

Aika na Nahreel ndio wamiliki wa lebo ya 'The Industry' ambayo inayowasimamia wasanii Wildad, Rosa Ree pamoja na kundi la Navy Kenzo.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com