Msanii wa Bongo Fleva na mpenzi wa Baraka the Price, Naj Dattani amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye hakumshauri mmewe kuachana na lebo ya RockStar4000 bali yalikuwa ni maamuzi yake.


Naji amesema Baraka sio mtu wa kushaurika kirahisi kwa mambo anayoyaamini yeye kuwa yanafaida kwake hivyo hata suala la kutemana na RockStar 4000 yeye hakumshauri chochote.

 “Sio kweli mimi Baraka sijawahi kumuingilia kwenye maamuzi yake na hata watu wanaomjua Baraka sio mtu wa kushauriwa sijui vitu vitu yaani anakuwaga na maamuzi yake, Sometimes hata kuna vitu vingine mimi mwenyewe huwa ninampinga lakini yeye akiamua kitu, ameamua”,amesema Naj huku akisisitiza kuwa amemsapoti yeye kujitoa RockStar 4000.

 “Mimi ofcourse ninamsupport na namuamini anajua anachokifanya na asingetoka kama angeona kuna faida kwake, na yeye ni mtu ambaye yupo serious na kazi zake na anaamini kwenye kipaji chake so hataki kutegemea kitu ambacho hakimuingizii faida kwake, so nikamuelewa na ninam’support na maamuzi yake”,amesema Naj kwenye mahojiano yake na TBC International.

Hata hivyo Naj amewathibitishia mashabiki wa Baraka The Prince kuwa kuna ngoma nyingi kali zinakuja hivyo wakae mkao wa kula.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com