Msanii wa muziki miondoko ya mduara nchini, AT amedai kuwa katika muziki wake haangalii ukubwa wa msanii kama umeimba hovyo kwenye ngoma yake basi hana budi kuifuta verse yako .

Mkali huyo kutoka zanzibar amesema hayo kupitia cloudsfm huku akimtaja msanii kutoka kenya 'Avril' ambae alishamfuta kwenye wimbo wake baada ya kuimba vibaya

. "Nilishaenda ogopa Dj kufanya wimbo na Avril lakini Avril aliimba utumbo mtupu mimi nilimtoa. Avril sio msanii sio kabisa yani sio msanii ambaye unategemea kumsikia halafu unamkuta kama vile alivyo Linah...no yani she very fake kabisa yani mpaka nimeshangaa nilikuwa najua jina lake ni kubwa anauwezo mkubwa lakini nimeenda kufanya nae wimbo aisee ni shughuli mpaka nimemtoa nimemuweka Alice wa THT na ngoma imekuwa kali lakini sijaitoa" alisema @at_original .

Aidha AT ameongeza na kusema kuwa yeye haangalii ukubwa wa jina la msanii bali anazingatia uwezo wa msanii na siku upepo wa promotion ukikaa sawa ataitoa ngoma hiyo ambayo alimtoa Avril (@theavieway) na kumuweka Alice wa THT.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com