Rapa wa kike ambaye anafanya poa katika muziki wa Hip hop, Chemical amefunguka na kusema aina ya wanaume ambao anatamani kuwa nao katika mahusiano na kusema yeye anavutiwa na watu kama kina Nay wa Mitego kwani yeye hapendi watu ambao ni masharobaro.

Chemical amesema hayo kupitia kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio na kudai yeye mpaka saizi bado yupo 'single' na hajaamua kuingia kwenye mahusiano kwa kuwa yeye anaamini katika mila na desturi.

"Mimi ni rapa lakini ni binti ambaye bado naamini katika mila na desturi kwa hiyo mpaka saizi bado nipo 'single' ila kama kuna mtu ambaye anaona anahitaji kuwa na mimi anapaswa kuja nyumbani na kufuata utaratibu, kwani naamini kuna sehemu wapo wanaume wa kweli ambao watatokea katika maisha yangu. Lakini pia mimi napenda wanaume fulani hivi wasiwe masharobaro ila wawe kama kina Nay wa Mitego hivi" alisisitiza Chemical

Chemical awali alishawahi kutokewa na rapa Stereo lakini alimtosa na kusema kuwa yeye anamuheshimu sana rapa huyo kama kaka yake na kusema ingekuwa ngumu kuwa naye katika mahusiano licha ya rapa huyo kuonyesha hisia zake wazi wazi kupitia vyombo vya habari.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com