Jerry Boniphace ‘Mesen Selekta’.

PRODYUZA wa Ngoma ya Hainaga Ushemeji ya Man Fongo, Jerry Boniphace ‘Mesen Selekta’ amesema kuwa, mastaa kibao wa Bongo Fleva aliokuwa akiwatengenezea ngoma wamemliza sana kwa kumlipa mkwanja kiduchu na wengine bure kabisa na kumsababishia kujikita kwenye muziki.
Akibonga na Over Ze Weekend, Mesen anayebamba na Ngoma ya Sukari akiwa chini ya Kampuni ya Dadid Investment alisema, kwa muda mrefu amekuwa akiwarekodia mastaa lakini kipato kiduchu alichokuwa akilipwa huku wengine wakitanguliza ushkaji kutokana na kazi hiyo aliokuwa akiwafanyia imemfanya kuwakimbia.
“Nimeona bora akili yangu ijikite zaidi katika kuimba japo nilikuwa sipo sana. Sasa nipo kamili na mashabiki wategemee ngoma juu ya ngoma kwa mwaka huu,” alisema Mesen ambaye pia ni mmiliki wa Studio ya De Fatality Music.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com