Kulikuwa na taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa kuwa muigizaji mkongwe wa Filamu na vichekesho Tanzania Amri Athuman maarufu kama King Majuto amefariki baada ya kuumwa taarifa hizo zimeelezwa kuwa sio za kweli.


Mchekeshaji maarufu Mboto Haji ambaye amefanya kazi kadhaa na Mzee Majuto ni miongoni mwa mastaa wa mwanzo kupata taarifa hizo na kulazimika kusafiri hadi Tanga nyumbani kwa mzee huyo ili kupata undani wa hali yake.


Kupitia kwenye Instagram yake leo July 23, 2017 Mboto amebainisha kwamba taarifa zilizokuwa zinasambaa kuwa King Majuto kafariki ni uzushi baada ya kufika nyumbani kwake na kumkuta angali hai.


>>”Baada ya kupata taarifa mbaya kuhusu mzee majuto nimelazimika kuja kwake tanga. Ni kweli anaumwa ila anaendelea vizur na sivyo kama watu walivyozusha kuwa mzee hatunae.


Kwa sasa mzee ni mzima nipo nae tanga” – Mboto.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com