Msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

 WANAMUZIKI ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo uitwao Utamu, Lulu Abas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa mwanamuziki wa kike anayempa mawazo hapa Bongo ‘sterss’ ni Vanessa Mdee ‘Vee- Money’ ambapo kila akifikiria juu ya kazi zake anajikuta akichanganyikiwa na kuzidi kukomaa kwenye gemu ili siku moja awe juu zaidi.

Mwanamuziki anafanya vizuri na wimbo uitwao Utamu, Lulu Abas ‘Lulu Diva’.

Akichonga na Uwazi Showbiz, Lulu alisema kuwa Vee Money ni mwanamuziki bora kwake na anauwezo mzuri sana ambapo ndoto zake ni siku moja kufanya muziki wa kimataifa kama ilivyo kwake ikiwezekana kabisa kumshinda, kwenda zaidi ya hapo alipo yeye kwa sasa.

“Bongo kwa wanamuziki wa kike kiukweli anayenipa stress ni Vee, kila mtu anafahamu kuwa ni mkali na anajituma kwenye muziki wake, sasa mimi malengo yangu ni kufanya kazi kwa juhudi ili kufika mbali, kwanza kuwa hapo alipo yeye na baadaye kupita zaidi,“ alisema Lulu Diva.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com