Muigizaji Kajala Masanja.

STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja hivi karibuni yalimkuta makubwa jijini Mwanza baada kunyofolewa kucha na wahuni alipokuwa kwenye majukumu ya kazi yake anayoifanya kwa sasa ya kampuni ya mchezo wa kubahatisha.

Akipiga stori na Risasi Jumamosi, Kajala alisema kuwa alikuwa kwenye harakati za kazi yake anayoifanya kwa sasa kwenye kampuni hiyo ambapo alikuwa akigawa tisheti ndipo mashabiki wakaanza kumvuta mkono mpaka kumbandua kucha aliyokuwa amebandika mkononi ambayo iliondoka na ukucha wake na kujikuta akipata jeraha na kumwaga damu nyingi.

“Yaani mimi nilikuwa sina ili wala lile nagawa matisheti mara wakaanza kunivuta kwa nguvu mpaka wakaitoa kucha yangu, hali hiyo ilinitesa asikwambie mtu jeraha la kucha linauma sana,” alisema Kajala.

Aliongeza kuwa, baada ya kucha yake kubanduka alitoa kilio kikubwa kwani alipata maumivu yaliyosababisha ashindwe kuendelea na majukumu yake.

“Maumivu niliyopata yalikuwa ni makali mno kiasi ambacho nilishindwa kufanya kazi yangu, nilipata matibabu ambapo kwa sasa naendelea vizuri,” alisema Kajala.

Msanii huyo amewaasa wasichana wenzake kuwa makini na kucha za kubandika kwani zikitoka kwa mtindo huo zinasababisha maumivu.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com