MUUZA nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ na mzazi mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, David Genz ‘Young D’, Mamisa Amir, wanadaiwa kuwa kwenye bifu zito kwa madai ya kuibiana mwanaume.


Chanzo makini kilidai kuwa, Mamisa ambaye awali alipojifungua alihifadhiwa na Jike Shupa, kwa sasa ni kama paka na panya, chanzo kikielezwa ni Mamisa kumpindua mwenzake kwa mwanaume wake japokuwa wenyewe wamekuwa wakifanya siri.


Baada ya kupata ubuyu huo, Risasi Jumamosi liliwatafuta wahusika ambapo lilianza na Mamisa ambaye alisema kuwa, hana tatizo na bishosti huyo na hata akikutana naye wanasalimiana.
Kwa upande wa Jike Shupa aligoma kuweka wazi huku akijiumauma na kusema: “Hata kama tuna bifu, ninyi kinawauma nini? Niacheni bwana.”

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com