Mtayarishaji wa muziki kutoka Mj Records, Daxo Chali amesema Wema Sepetu ni 'noma' katika uimbaji, kwani hakutegemea kama angekuwa na uwezo huo mkubwa katika kiasi hicho.

Daxo Chali alisema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio  na kuongeza kuwa kupitia kazi mpya ya msanii Haitham ambaye yupo chini yake, Wema Sepetu ameonyesha uwezo wa hali ya juu.

"Niliona wimbo wa Haitham unahitaji mtu nikafikiria nifanyaje, lakini wakati huo huo nilikuwa na mpango wa kuja kufanya wimbo ambao ningependa kuona Wema Sepetu anakuwepo, basi kwenye huu wimbo mpya wa 'Play boy' nikaona huyu humu atakaa". Amesema  Daxo

Basi harakati za Daxo kumsaka mwanadada Wema Sepetu zikaanzia hapo

"Nikaanza kumtafuta Wema Sepetu, kuna siku kweli akafika na kufanya. Wema Sepetu anajua sana kuimba watu wengi hawajui hilo, sema tu hizo 'melody' ndiyo zilimsumbua maana ni za kiswahili lakini zinaimbwa kama kifaransa lakini kwingine amenyoosha". Amefunguka Daxo Chali

Hii ni mara ya pili kwa Wema Sepetu kuingia studio, kazi ya kwanza ya Wema Sepetu alishirikishwa na msanii Snura Majanga wimbo ulikuwa unaitwa 'Shoga yake mama' na wimbo wa pili ni huu wa msanii Haitham kutoka Mj Records ngoma inaitwa 'Play boy'
 Facebook  Twitter  Google+

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com