Siku chache baada ya mwimbaji wa Bongofleva na kiongozi wa WCB, Diamond Platnumz kuachia video ya wimbo mpya ‘Eneka’ mashabiki na wafuatiliaji wa muziki wa Bongo wanadai kuwa wimbo huo unafanana na wimbo wa mwimbaji staa wa Nigeri Davido unaoitwa ‘Fall’.

Kutokana na stori hizo kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii Ayo TV na millardayo.com zimemtafuta producer ambaye alihusika kutenegeneza wimbo huo kutoka WCB, Lizer ambapo amefunguka kutolea ufafanuzi juu ya madai hayo ya Eneka kufanana na Fall.
”Kwanza naweza nikasema hivi huu ni muzuki na muziki pia una style yake inategemea ni muziki wa aina gani unaweza ukafanana. Nimesikia hizo habari kwamba wimbo wa Eneka unafanana na Fall ya Davido lakini naomba kitu kimoja watu waelewe kwamba muziki wa Kimarekani umechanganywa na kiafrika lakini vitakavyobadilika vitabadilika vichache.

“Tusiwe waongo, sisi tunafuata Nigeria wanafanya nini, tusiwe wanafiki kwamba tusiangalie Nigeria wanafanya nini kwa sababu wametutangulia. Kwa hiyo ili tufike kule walikofika wao lazima tupite njia ambazo wanapita wao.
  
“Sioni ajabu kwamba mtu akisema hii imefanana…mi ninachojali ni kwamba watu watapokeaje nyimbo, itapendwa au itafanya vizuri. Hicho ndicho ninachokiangalia zaidi.” – Lizer.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com