Shalom watu wa Mungu!

Mtumishi mmoja kaandika hapa juu ya zaka: unaweza usimuelewe sana ama usimpende, lakini ana ujumbe wa muhimu...Soma Hapa;

SADAKA YA AJABU KULIKO ZOTE:-

Kuna sadaka inaitwa Fungu la kumi (Zaka/Tithe) ambayo unatakiwa kutoa asilimia 10 ya mapato yako yote. Sadaka hii umaajabu wake uko hapa:- usipoitoa kwa HIARI itakutoka kwa LAZIMA.

KIMSINGI....

Hii sadaka unapoitoa inafanya kazi kubwa mbili:-

1). Inalinda na kuhifadhi usalama wa mambo yako yote:- (biashara yako, afya yako, ndoa yako, watoto wako, afya za wanaokutegemea, usalama wa mali zako n.k)

2). Inafungua madirisha ya baraka:- (yaani unakuwa na ideas nyingi useful, unakuwa na uwezo wa kubuni na kutekeleza, unakuwa na nguvu ya pekee kufanya kazi, unakuwa na maono, unakuwa na kibali kwa kila ulifanyalo). [MALAKI 3:8-12]

CHA AJABU....

Kwa kuwa kazi ya sadaka hii ni kukulinda, usipoitoa kwa hiari tena kiukamilifu, maana yake ni kwamba ule ulinzi unakuwa haupo. Ndio utashangaa umeuchuna kutoa hilo fungu la kumi let say elfu themanini (katika laki nane unayolipwa), halafu unapigiwa simu kwamba mzazi anaumwa kijijini na unakwenda kutumia laki mbili! 

Ama ndio ile unagoma kutoa fungu la kumi then unashangaa kila mshahara ukitoka ama kila ukishika fedha, matatizo yanaongozana msururu, kufumba na kufumbua unakuta hela zimeisha bila hata kujielewa elewa! Kama una tatizo katika ndoa yako, kabla hujaomba ama kuombewa hebu kagua ikiwa unatoaga fungu la kumi kiuaminifu.

Huwezi kuacha kutoa fungu la kumi kwa uaminifu halafu uchumi wako ukabaki salama. Huwezi ukaacha kutoa fungu ka kumi halafu uwe na garantii ya kwamba ndoa yako itakuwa ni, "heat free marriage", "stress free marriage", ama "Haeaven on Earth" marriage. Haiwezekani!

Na kama huwa hutoi fungu la kumi na unadhani kuwa uko salama, huenda hujajua kwamba kutotoa kwako ndio kunasababisha mambo yako yawe magumu kifedha ama yawe yanaenda kwa jasho jingi sana. Kama unatoa fungu la kumi kiuaminifu hutakiwi kuwemo katika orodha ya wanaopambana na joto la fedha kuwa ngumu mtaani. Nakuona unajitetea moyoni kutokana na kutotoa kwako. Pleaseee hebu jaribu kuitoa hii sadaka kwa uaminifu ujionee inavyothibitisha kile anachosema Mungu kuhusu sadaka hii.

HALAFU...

Huo unaoufanya ni utoto ujue! Yaani Mungu anakupa milioni moja unakuwa mchoyo kumpa laki moja?!!?!!? Hivi unajua kwamba Mungu hafanyagi madili makubwa/ya maana na watoto? Unajichelewesha na kujiangamiza ujue? 

Hakuna maombi wala matamko ya kinabii yatakayokufanikisha kiuchumi, kindoa, kiuzazi, kikazi ikiwa hautoi fungu la kumi kwa bidii, kwa furaha na uaminifu. Hata kama unatafuta mtoto, mume, ajira (n.k) unapoendelea na maombi ama kuombewa tafadhali zingatia sana fungu la kumi. Sadaka zote unazotoa zinaanza kuwa na maana ukishakuwa umemalizana na Mungu katika kipengele cha fungu la kumi.

Na kama hutoagi fungu la kumi wala hata usijichoshe kumuomba Mungu kwamba akubariki kiuchumi. Tena uelewe kwamba suala sio kiwango, suala ni moyo. Kama unaona ni ngumu kutoa fungu la kumi katika laki moja unayopata sasa, usifikiri ukishika milioni utaweza kutoa, kinachokuzuia sasa na laki moja ndicho kitakuzuia mbeleni na milioni kumi.

USISAHAU...

Mimi sikuelezi habari nilizozisoma ama kujifunza tu, hapana! Ninakueleza uzoefu halisia kutoka katika maisha yangu. Ninarekodi ya majanga na misala iliyonipata kwa kupuuza fungu la kumi ama kutotoa kwa uaminifu na ninazifahamu baraka za kuzingatia fungu la kumi kwa uaminifu. Nilishaweka agano na Mungu ya kwamba sitakaa nicheze na habari ya fungu la kumi, maana kibano chake sio cha hapa! Kama unabisha, shauri yako, endelea kuhanya hanya hivo hivo!

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com