STAA wa sinema za Kibongo, Flora Festus Mvungi, kwa mara nyingine amejikuta akipatwa na kigugumizi cha kushindwa kujibu swali lililomtaka kufafanua juu ya kinachoendelea kwenye ndoa yake na mwanamuziki Hamis Ramadhan ‘H-Baba’ kufuatia tetesi za ndoa hiyo kuwa haipo tena.

Katika mahojiano na Wikienda maeneo ya Urafiki, Dar, wikiendi iliyopita, Flora ambaye amezaa watoto wawili na H-Baba, alijikanyaga baada ya kuulizwa kinachoendelea kwenye ndoa yake ambapo badala ya kujibu swali hilo alimtaka mwandishi wetu aulize mambo mengine na si masuala ya ndoa.

“Mimi niko huku (Dar), Hamis (H-Baba) yuko huko Mwanza, sasa hayo mengine sitaki kusema, kwa sasa niko bize na masomo ya Afisa Uhusiano wa Umma (Public Relation Officer), sitaki maswali ya ndoa, ila…., ilaaaa…. Lakini maisha yapo na yanasonga kama kawaida. Nakuomba uulize mambo mengine lakini siyo hilo,” alisema Flora ambaye ndoa yake na H-Baba ya miaka kadhaa ilijaa mbwembwe nyingi kabla ya kudaiwa kupigwa na kimbunga.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com