David Adeleke ‘Davido’.

MKALI wa ngoma ya Fall, David Adeleke ‘Davido,’ hivi karibuni amenusurika kuchezea kichapo kutoka kwa kundi la wahuni waliomvamia ndani ya klabu moja ya usiku huko London, Uingereza alikokwenda kwa ajili ya kula bata na wapenzi wa kazi zake za muziki.

Baada ya tukio hilo la kuvamiwa na wahuni hao kumtokea, Davido alipopata upenyo alitoroka klabuni hapo kwa kutumia mlango wa nyuma lakini pia chanzo cha fujo hizo hakikuweza kujulikana.

Hata hivyo, baadaye jamaa mmoja anayetambulika kwa jina la Mrchrisonline kwenye Ukurasa wa Instagram, aliandika ‘post’ na kuielekeza kwa Davido iliyosomeka; “We mjinga umekuwa na bahati sana usiku wa jana. Hii ni London siyo Nigeria na usingetokea mlango wa nyuma ungetuelewa mlangoni.” Lakini Davido hakuweza kuijibu post hiyo.
Lagos, Nigeri.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com