STAA wa kitambo wa Bongo Movies, Chuchu Hans amefunguka kuwa, baada kupata mtoto aitwaye Jaden na staa mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’, kwa sasa hakuna anayewazia ndoa kati yao, badala yake kila mmoja anafikiria kuhusu malezi ya uzao wao huo.

Chuchu aliliambia Wikienda kuwa, yeye na Ray hawajakaa na kulizungumzia suala la ndoa lakini anaamini kuwa siku ikifika mambo yatakuwa bambam.

“Hakuna hata mmoja kati yetu anayeiwazia ndoa. Sasa hivi kila mtu jicho lake lipo kwa mtoto na naamini siku ikifika Ray mwenyewe atazungumza kwa kuwa jambo hili halitaki kulazimishwa hata siku moja,” alisema Chuchu.

Ungana nasi Facebook Like page yetu hapa chini

Weka Maoni Hapo Chini Kuhusu Habari Hii

Facebook Blogger Plugin by Celebrity Swaggz

Post a Comment

 
Top