Msanii Alikiba amefunguka kwa kudai Baraka the Prince umri unamsumbua na ndiyo maana muda mwingine wanamuacha pembeni pekee yake japo akielezwa kitu huwa anarekebishika.

Kiba amebainisha hayo baada ya kuenea tetesi za muda mrefu kuwa Baraka na Ommy hawana mahusiano mazuri japo kwa sasa hivi wapo katika 'label' moja ya 'Rockstar4000' inayowasimamia kazi zao muziki.

"Baraka muda mwingine unajua tena umri tu unamsumbua lakini yuko vizuri akielezwa anasikiliza na kurekebishwa. Lakini kiukweli mtoto akifanya kosa si unamwambia bwana, unamfundisha kwa hiyo ni mdogo wetu tunamuelimisha kwa vitu kama hivyo na sidhani kama anamchukia Ommy Dimpoz labda katika maneno tu ya kawaida ya mtaani", amesema Kiba.

Pamoja na hayo, Alikiba amesema muda wowote kuanzia sasa ataachia ngoma yake mpya kwa madai amesha rekodi nyimbo nyingi na zipo ndani tayari kwa kutoka.

Hata hivyo siku za hivi karibuni  Alikiba alitangazwa rasmi kuwa 'Director of Music and Talents' pamoja na kuwa mmiliki wa kampuni ya 'Rockstar4000 Music Entertainment Co & Rockstar Television' (share holder).

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com