Msanii Alikiba ambaye siku za karibuni aliahidi kuachia ngoma yake mpya amefunguka na kusema baada ya kuachia ngoma hiyo inayosubiriwa na mashabiki zake kwa hamu atatambulisha wasanii walio chini ya 'Label' yake Kings Music.

Alikiba amesema kwa sasa anawajenga hao wasanii waliopo chini ya uongozi wake huo ili waweze kufanana na yeye kwa mambo mengi na waweze kupata mafanikio kupitia muziki ambao wanafanya.

"Nina label yangu inayofahamika kama 'Kings Music' lakini naweza kusema haijaanza kufanya kazi kwani toka nimerudi na kusimama kwenye muziki sijawahi kutoa msanii kwenye label yangu lakini saizi baada ya kutoa wimbo wangu mpya nitaanza kutoa ngoma kutoka kwa wasanii wangu kwani maandalizi yameshafanyika na videos tushafanya, ngoma ziko sawa na wasanii wenyewe wako vizuri. Nimewaanda wasanii wangu jinsi ambavyo mimi nipo nataka na wao wawe hivyo hivyo, wawe watu wa watu, wapendwe na watu, wawe na mashabiki wa kutosha yaani mimi nambadilisha mtu kwa lengo zuri" alisema Alikiba

Alikiba anasema muda wowote ule anaweza kuachia kazi hiyo mpya kwani sasa kilichobaki ni kusema siku gani kazi hiyo itaachiwa kwani kila kitu kimeshakamilika hivyo anasubiri siku tu waweze kuachia kazi hiyo, ambayo inaonekana kusubiriwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa Alikiba.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com