DAR ES SALAAM: Baada ya kutofautiana na mastaa wenzake kwenye sakata la maandamano ya kupinga filamu za nje waliyofanya baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi, mchekeshaji Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amewatolea maneno ya shombo.

Steve aliliambia Wikienda kuwa, aliamua kujitenga na baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi kwa sababu hawezi kukaa nao ndiyo maana ameanzisha kundi lake ambalo ni la watu wenye akili, wanaoweza kufanya mambo ya maana na ya kuleta mafanikio.

“Ningeendelea kujumuika nao, ningekuwa mjinga kama wao. Kwanza mimi ndiye maarufu kuliko wao maana nina kipaji cha kuzaliwa, lakini wao wamejifunza, maisha yangu ni mazuri tofauti na wao ambao hata milioni tatu kwao kupata ni shida,” alisema Steve.

Ungana nasi Facebook Like page yetu hapa chini

Weka Maoni Hapo Chini Kuhusu Habari Hii

Facebook Blogger Plugin by Celebrity Swaggz

Post a Comment

 
Top