Msanii anayewakilisha kanda ya kati, Moni Centrozone ametoa ya moyoni kamwe hawezi kumtenga msanii Roma kwa sababu alipata matatizo hivi karibuni kwani ni mtu aliyemshika mkono kwenye 'game' ya bongo fleva.

Moni kupitia kamera za eNewz amejibu tetesi za watu wanaodai kwamba amejiweka mbali na msanii Roma tangu walipopata matatizo ya kutekwa na watu wasiojulikana kwa siku tatu kwa kujibu siyo kweli kwani wao ni zidi ya marafiki hivyo ni vigumu kutengana.

"Roma ni damu yangu, ni kaka yangu ambapo kama siyo yeye nisingefika mapema kwenye 'mainstream' n amaanisha ningechelewa kujulikana. Hata siku moja sijawi kufikiria kujitenga naye kwa sababu yeye kapata matatizo. Mimi nimetoa ngoma kwa sababu natakiwa kutoa na yeye bado anasubiri apone vizuri arudi kazini kwani bado tuna kazi nyingi za kufanya muda mfupi tuu baada ya kurejeshwa kwa studio ya Tongwe" - Moni alielezea.

Moni kwa sasa ana-'hit' na wimbo unaokwenda kwa jina la tunaishi nao alioutoa muda mfupi baada ya kurejea uraiani tangu alipotekwa na watu wasiojulikana akiwepo yeye, Roma na Prodyuza Bin Laden na msaidizi wa ndani.

0 comments:

Post a Comment

 
Top
CelebritySwaggz.Com